Jioni Njema; Man United wasafishiwa njia kwa Matic # Mbappe kuivunja ‘BBC’ Madrid # Leipzig wajiandaa kumuuza Keita

MANCHESTER- MANCHESTER United imebaki peke yake kwenye mbio za
kumsajili kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, baada ya wapinzani wao, Juventus
kuelekeza nguvu zao kwa Blaise Matuidi wa PSG.
Mchambuzi wa soka
Hispania, Guillem Balague amesema Real Madrid imevujisha siri kuwa, Kylian
Mbappe atakua klabuni hapo iwapo mmoja wa wachezaji wanaounda kombinesheni
maarufu BBC atauzwa. BBC ni Bale Gareth, Benzema Karim na Cristiano Ronaldo.
Hata hivyo, Madrid imesema Mbappe anaweza kuja bila kubughudhiwa kwa BBC.
Gazeti maarufu Ujerumani,
Bild, limeripoti kuwa klabu ya RB
Leipzig inajiandaa kimya kimya kuziba pengo la Naby Keita anayetarajiwa kuhamia
Liverpool. Limeeleza kuwa Mkurugenzi wa Michezo, Ralf Rangnick amewatuma skauti
watafute mbadala wa kiungo huyo.
Kwa mujibu wa mmoja wa
watangazaji wa Radio Catalan ya mjini
Barcelona, Gerard Romero, klabu ya mji huo, Barcelona tayari imekubaliana
maslahi binafsi na Philippe Coutinho wa Liverpool na kilichobaki ni kukamilisha
dili na Liverpool.
Makamu wa Rais wa Monaco,
Vadim Vasilyev amesema wanafanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na mshambuliaji
wao, Kylian Mbappe. Pia kiongozi huyo amebainisha kuwa wachezaji wawili Thomas
Lemar na Fabinho, hawaendi kokote licha ya kuhusishwa na kuondoka.
Inter Milan imesema
iko tayari kufanya biashara na Manchester United, kuhusu uhamisho wa Ivan
Perisic. Bosi wa Inter, Luciano Spalletti amesema dili hilo lenye thamani ya
pauni milioni 48 () litafanyika muda wowote. Sky Sports.
No comments