Takukuru yawakamata wagombea wa TFF
MWANZA- BAADHI ya wagombea wa nafasi mbalimbali za
uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa soka,
wamekamatwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za
kujihusisha na rushwa jijini hapa.
Akizungumza kuhusu
kukamatwa kwa watu hao, Msemaji wa Takukuru, Ernest Makale alisema watu hao
walikamatwa baada ya kufuatiliwa nyendo zao na kubaini dalili za uwepo wa
rushwa.
Makale
aliwataja waliokamatwa kuwa ni, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam
(DRFA), Almas Kasongo, Shafii Dauda, Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam
Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma pamoja na Kelvin Shevi.
“Tumewakamata, kwa sababu hiki siyo kipindi
cha kampeni na dalili zote kwamba walikuwa hapa kwa ajili ya uchaguzi
unaotarajiwa zilikuwa zipo wazi,”
“Kama Takukuru tumeona kuwa, kuna viashiria
vya rushwa na ndipo tukaweka mitego yetu kwenye sehemu walizokuwa wanaendeshea
vikao vyao vya siri ndipo tulipoweza kuwakamata,” alisema
Makale.
Pamoja na hayo, Makale alisema watuhumiwa hao waliachiwa kwa dhamana ila wanaendelea na uchunguzi wao endapo watakapopata ushahidi wa kutosha watafikishwa mahakamani.
Pamoja na hayo, Makale alisema watuhumiwa hao waliachiwa kwa dhamana ila wanaendelea na uchunguzi wao endapo watakapopata ushahidi wa kutosha watafikishwa mahakamani.
Chanzo; EATV
No comments