Jioni Njema; Man United haina mpango na Bakayoko # Rooney apewa jezi no. 10 # Hakuna dili lolote la Chamberlain # West Ham wajiondoa kwa Hart

LONDON- MANCHESTER
United, imesema kwamba hawana mpango wa kumsajili windo la Chelsea, Tiemoue
Bakayoko kwa ajili ya matumizi ya msimu ujao.
Licha ya awali kudaiwa
kutaka kumsajili, klabu hiyo imekanusha na kudai kuwa haina pango huo. hayo
yanasababisha mpango wa Chelsea wa kumsajili kiungo huyo, kupata nguvu zaidi na
kuwa mchezaji wa tatu baada ya Willy Caballero na Antonio Rudiger.
Mshambuliaji mpya wa
Everton, Wayne Rooney amepewa jezi namba 10, huku mchezaji mwingine mpya,
Sandro Ramirez akipewa jezi namba 9 na namba 1 ikienda kwa mlinda mlango mpya,
Jordan Pickford.
Arsenal imesema kuwa
hakuna dili lolote ambalo limekubaliwa na timu hiyo, kutoka timu yoyote kwa
ajili ya kumsajili winga wao, Alex Oxlade-Chamberlain.
West Ham United
imesema kuwa haina tena mpango wa kumsajili kipa wa Man City, Joe Hart, baada
ya timu hiyo kukataa mpango wa Hammers wa kumchukua kwa mkopo wenye kipengele
cha kumsajili baada ya mkopo kuisha.

Wagonga Nyundo wa
London, West Ham, wamesema kinda wao hatari wa Georgia, Domingos
Quina ananyatiwa na timu kadhaa ikiwemo Arsenal.

Mwenyekiti wa klabu ya
Bayern Munich, Karl-Heinze Rummenigge amesema kuwa amefurahishwa na ujio wa
James Rodriguez, kutoka Real Madrid ya Hispania.
“Kama timu,
tumefurahishwa zaidi na ujio wake na kufanikisha usajili huo. kumsainisha
Rodriguez ilikuwa ni hitaji kubwa ambapo alitaka kuungana naye tena baada ya
kufanya naye kazi Madrid,” alisema Rummenigge.

Klabu ya Valencia ya
Hispania, imesema kuwa imemfungia kazi kiungo wa Chelsea, Kurt Zouma na
inatarajia kufanikisha dili hilo muda wowote na kuipata huduma yake kwa ajili
ya msimu ujao wa La Liga.
Habari zote na Sky
Sports.
No comments