Jaribio la kifaa cha kuwalinda wanawake dhidi ya Ukimwi lafanikiwa

PARIS- WATAFITI
nchini Marekani, wamesema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia
mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya Ukimwi (VVU) limefanikiwa.
Utafiti
zaidi sasa utafanywa kwa vijana barani Afrika. Katika utafiti huo, wasichana
walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na Ukimwi, ambao ulibadilishwa
kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.
Ni mojawapo
ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho, wanawake watatumia kujilinda dhidi ya
maambukizi ya VVU ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.
Wakiripoti
ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya VVU mjini hapa, watafiti hao walisema wanafurahi
kwamba wasichana hao walitumia kifaa hicho na kusema kuwa wamekipenda.
Wanawake na
wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24, wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya
visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.
Takriban
wanawake 1,000 huambukizwa virusi kila siku katika bara la Afrika hususan
katika mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.
BBC.
No comments