Mezani Jioni; Monaco haijamuuza Mbappe # Liverpool yamrudia Keita # Neymar kuondoka Barca
MADRID- MONACO
imeiambia Sky Sports kwamba, hawajakubaliana kwa namna yoyote na Real Madrid kuhusiana
na dili la kumsajili Kylian Mbappe (18) na kukanusha uvumi kuwa wamekubaliana kiasi
cha pauni milioni 160 (sh bilioni 464). Sky Sports.
Hatima
ya mshambuliaji wa Barcelona na Brazil, Neymar (25) iko shakani, kutokana na
vyanzo vya karibu na mchezaji huyo kudai kuwa mchezaji huyo ataenda PSG. Vyanzo
hivyo vinadai kuwa, kuna uwezekano wa asilimia 90, Neymar kuhama kukimbia
kivuli cha Lionel Messi. Sky Sports.
Kwa
mara nyingine tena, Liverpool imewasilisha dau la pauni milioni 74 (214.6),
mezani kwa klabu ya RB Leipzig, kwa ajili ya kumsajili kiungo mahiri wa timu
hiyo, Naby Keita (22) baada ya kukataliwa mara mbili awali. Daily Star.
Barcelona
wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya pili kwa Liverpool, ili kuruhusiwa kumnunua
kiungo mahiri, Philippe Coutinho (25) baada ya ofa yao ya kwanza ya pauni
milioni 72 (sh bilioni 208.8) kukataliwa. Hata hivyo, bosi wa Liverpool, Jurgen
Klopp amesema mchezaji huyo hauzwi. Sky
Sports.
Baada
ya kushindwa kumsajili Fabinho kutoka Monaco, matajiri wa Paris, PSG
wameelekeza fedha zao kwa kiungo wa Porto ya Ureno, Danilo Pereira (25). Hata hivyo,
Porto wana uhakika wa kuingiza pauni milioni 60 (sh bilioni 174) kama ada ya
kumuuza mchezaji huyo. Le10Sport.
Inter
Milan inaripotiwa kuandaa dau la pauni milioni 15 (sh bilionii 43.5), kwa ajili
ya kumsajili winga wa Tottenham Hotspurs, Erik Lamela (25) lakini Spurs
wanataka pauni milioni 18 (sh bilioni 52.2). Sky Sports.
Riyad
Mahrez anaendelea kufanya mazoezi na wenzake kama ilivyo kawaida, licha ya
kuwepo kwa taarifa kuwa Roma imewasilisha dau lililoboreshwa na kufikia pauni
milioni 30 (sh bilioni 87), baada ya dau la kwanza kukataliwa. Sky Sports.
No comments