Header Ads

Israel yaondoa hatua zote za kiusalama Jerusalem



Lorry removes scaffolding from outside Jerusalem holy site (27/07/17)

TEL AVIV- SERIKALI imeamua kuondoa hatua zote za kiusalama, ambazo zilikuwa zimewekwa ndani ya eneo lote takatifu la Msikiti wa Al Aqsa jijini Jerusalem.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, hatua hizo zimeondolewa ili kusitisha maandamano ya Wapalestina ambao walikuwa wakipinga hatua hiyo ya Serikali.
Mara baada ya kuondolewa kwa hatua hiz, viongozi wa dini katika utawala wa Palestina walisema kwa sasa wataacha kususia eneo hilo takatifu.
Vizuizi hivyo viliendelelea leo asubuhi, siku mbili baada ya mitambo ya kutambua chuma kuondolewa. Vifaa hivyo viliwekwa, baada ya tukio la kuuawa kwa polisi wawili wa Israel katika eneo hilo na mtu ambaye aliingia na silaha.
Israel imesema kuwa itachukua hatua zisizokuwa na vizuizi miezi sita inayokuja.
Kumekuwa na karibu makabiliano ya kila siku kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamanaji, tangu mitambo ya kutambua chuma iwekwe baada ya kuuwawa kwa polisi Julai 14 mwezi huu karibu na eneo linalofahamika kama Haram al-Sharif kwa Waislamu na Temple Mount kwa Wayahudi.
Wapalestina wanne waliuawa na raia watatu wa Israel kuuliwa, kwa kuchomwa visu na Mpalestina ambaye alidai alikuwa akilipiza hatua za Israel eneo takatifu.
BBC

No comments

Powered by Blogger.