Lisu: Tutaendelea kumkosoa JPM
DAR ES
SALAAM- SAA chache baada ya kuachiwa kwa dhamana huku akiwa amesota rumande kwa
siku saba, Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Rais wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesema wapinzani wataendelea
kuzungumza na kumkosoa Rais John Magufuli.
Akisisitiza
kuwa kifo ndiyo njia pekee ya kuzuia hilo lisitokee, amesema: "Wanataka
tunyamaze ili waendeshe nchi hii wanavyotaka wao. Taifa hili ni la mfumo wa
vyama vingi, tuna haki ya kufanya mikutano, tuna haki ya kufanya maandamano na
tuna haki ya kutoa maoni yetu.
“Kwa msingi
huo hakuna wa kutunyamazisha nchi hii si mali ya mtu binafsi.
Alisema
hayo jana katika mkutano wake na wanahabari, muda mfupi baada ya kupewa dhamana
akibainisha kuwa kukamatwa na kuwekwa mahabusu na hata kufungwa, hakutamzuia
kusema na kumkosoa Rais kwani akiwekwa mahabusu au kufungwa, atazungumza akiwa
kifungoni.
"Ukisema
tu unakumbana na Segerea ili tumwachie yeye peke yake, hatutamwachia. Hakuna
gereza litakalotunyamazisha … atupeleke mahabusu kwa sababu tutazungumza tukiwa
huko, hata akitufunga tutasema tukiwa kifungoni,” alisema.
"Njia
rahisi ya kwenda mbinguni ni kupinga uonevu, itabidi tufe kwanza ili tusiseme,
mwambieni Magufuli tutanyamaza tukiwa wafu kwa sababu wafu hawasemi".
Alibainisha
kuwa kunyamaza kunaweza kusababisha nchi kuangamia, na kwamba hakuna atakayewanyamazisha.
No comments