Gari lenye bango la kampeni za Joho lakamatwa operesheni dawa za kulevya Mombasa
MOMBASA-
POLISI wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya mjini hapa, wanashikilia
gari yenye mabango ya kampeni ya Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ambayo
ilikamatwa katika mtaa wa Nyali ikihusishwa na dawa hizo.
Mkuu wa
Polisi mjini hapa, Larry Kieng alisema gaari hilo lilikamatwa kwenye msako
maalum pamoja na watuhumiwa watatu wa dawa za kulevya waliokuwa wakitafutwa kwa
muda mrefu wakiwa na dawa zenye thamani ya mamilioni ya shilingi.
Aidha,
wapelelezi hao wa polisi walifanikiwa kukamata kiasi cha fedha cha shilingi
milioni 4.5 za Kenya na dola za Marekani 10,000 ambazo zinaaminika zilikuwa
zikitumika kwenye uagizaji na usambazaji wa dawa hizo.
“Ni kweli
tumelikamata gari hilo lenye mabango hayo, ambayo yanamnadi Joho. Lakini hatutaweza
kusema kwa sasa kuwa gari hilo ni lake, hadi hapo tutakapopata vithibitisho
kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) kwani tumewasiliana nao,” alisema
Kieng.
Kieng alisema
watuhumiwa hao walitambuliwa kuwa ni Abdullahi Ahmad Kheri (raia wa Tanzania),
Hope Mbaga na Musa Kihara ambao wote ni Wakenya.
Gari hilo
lilikuwa lilikamatwa likiwa limesihifadhiwa kwenye yadi ya moja ya majengo
yanayomilikiwa na watuhumiwa hao.
The Star.
No comments