Header Ads

Diwani abainisha sababu viongozi wa Chadema kujiuzulu



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXiQHi0-ThZvSxDHVdFSJZduNANrfoP6Z_B7FAYMmQRz6ru3Upi9SGdQz5WCkCLJLfi6AxaYpqkuqqtj5CI_V8RK8CVfr5QjlbAwUQw0X7EP5_jMPKy8oXZrvLRMVDmq_gJxXjuLzmdMs/s1600/DSC05462.JPG

ARUSHA- DIWANI wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye amejiuzulu, Edward Moita amesema utaratibu mgumu ndiyo chanzo cha viongozi wengi wa chama hicho kujiengua mkoani hapa.
Moita ambaye alikuwa diwani wa kata ya Moita iliyopo wilaya ya Monduli, alisema inawawia vigumu madiwani na viongozi wa chama hicho kushirikiana na watendaji wa Serikali kwani wanaonekana wasaliti.
Alisema anachojua yeye ni kwamba, pamoja na kuwa kiongozi kwenye chama cha upinzani anapaswa kushirikiana na watendaji walioko madarakani kutatua kero za wananchi lakini ushirikiano huo unaonekana kuwa batili na usaliti.
Baadhi ya wananchi wakiwemo wa kata hiyo, wamesema wametofautiana mitazamo juu ya kujiuzulu kwa madiwani hao  ambapo baadhi yao wamefurahia na wengine wakisema wanachotaka ni kuona matatizo yao yanapata ufumbuzi na wanakuwa na maendeleo.
Kabla ya kujiuzulu Moita ambaye ni wa saba mkoani hapa, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Chanzo; Redio One

No comments

Powered by Blogger.