Header Ads

Kombora la Korea Kaskazini linaweza kufika Marekani

Korea Kaskazini ilitoa picha za kombira hilo la masafa marefu ICBM likirushwa

WASHINGTON DC- MAREKANI imethibitisha kwamba Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu (Hwasong -14), ambalo kulingana na wataalama wanaamini linaweza kufika katika jimbo la Alaska nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje nchini, Rex Tillerson amelitaja jaribio hilo kuwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia na kuonya kwamba Serikali haitakubali hatua ya Korea Kaskazini kujihami na nyuklia.
Korea Kaskazini imedai jana kwamba, ilifanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ICBM. Wakijibu, Marekani na Korea Kusini zilirusha makombora Kusini mwa maji Korea.
Zoezi hilo la kijeshi la pamoja lililenga kuonesha uwezo wa mashambulizi ya mataifa hayo mawili, Pentagon ilisema. Ijapokuwa jaribio la jana lilionekana kuwa hatua kubwa, wataalam wanaamini kwamba Korea Kaskazini haina kombora la masafa marefu la kinyuklia.
Tillerson, pia alionya kwamba taifa lolote ambalo linasaidia kiuchumi na kijeshi Korea Kaskazini ama limefeli kuidhinisha kwa ukamilifu maamuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa, linasaidia utawala hatari.
Marekani imetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili suala hilo. Mkutano wa faragha wa wanachama wa baraza hilo, unatarajiwa baadaye leo.
Je Korea kaskazini ilisema nini jana?
Tangazo katika runinga ya taifa ya Korea Kaskazini lilisema kuwa, kombora hilo aina ya Hwasong -14 linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine lilisimamiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Ilisema kuwa kombora hilo liliruka umbali wa kilomita 2,802, na kusafiri kwa umbali wa kilomita 933 kwa dakika 39 kabla ya kuanguka baharini.
Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia, ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneo lolote duniani.
Shirika la Habari cha Korea Kaskazini (KCNA), baadaye lilimnukuu Rais Kim Jong-un akisema kuwa jaribio hilo ni zawadi kwa Wamerakani siku yao ya uhuru. Jaribio hilo ambalo ni miongoni mwa majaribio ya makombora yake, linakiuka marufuku ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Lakini wataalam wengi wanaamini kwamba, Korea Kaskazini bado haijakuwa na uwezo wa kutengeza kichwa cha kinyuklia kinachoweza kutosha katika kombora la masafa marefu na kwamba kombora kama hilo haliwezi kushambulia eneo linalolenga.
Je kombora hilo lina uwezo wa kusafiri umbali gani?
Swali kuu ni linaweza kusafiri kwa umbali gani, alisema mwandishi wa BBC Evans Seoul.
Je linaweza kushambulia Marekani?
David Wright, kutoka muungano wa kisayansi anasema kuwa iwapo ripoti hiyo ni ya sawa, kombora hilo linaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita 6,700.
“Umbali huo unaweza kulifanya kufika Alaska, lakini sio visiwa vya Hawaii ama hata majimbo mengine 48 ya Marekani. Siyo kombora la pekee ambalo Korea Kaskazini itahitaji,” alisema.
Pia aliongeza kuwa, ni lazime taifa hilo liwe na uwezo wa kulinda kichwa cha nyuklia kinapopaa angani na sio wazi iwapo lina uwezo huo.
BBC

No comments

Powered by Blogger.