Breaking; Lissu apata dhamana atakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam
DAR ES SALAAM- MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia leo asubuhi kwa dhamana ya Shilingi milioni
10 Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Chadema,
Tundu Lissu.
Aidha, Mahakama hiyo
imemuamuru Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki, kutotoka nje ya Dar es
Salaam kama moja ya masharti ya dhamana hiyo ya kesi hiyo.
Dhamana hiyo inakuja
kufuatia ombi la mawakili wa Serikali, la kuiomba mahakama imnyime Lissu dhamana
kutupiliwa mbali na Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri.
Julai
24, Mbunge huyo alinyimwa dhamana na kutakiwa abaki rumande hadi leo ambapo
Mahakama itatoa uamuzi wa dhamana, kutokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha
pingamizi.
Mahakama
hiyo ilifikia uamuzi huo, baada ya mawakili wa Lissu, Fatma na wa Serikali,
Mutalemwa Kishenyi na Saimon Wankyo kujibizana kwa hoja kwa zaidi ya saa mbili.
Baada
ya majibizano hayo, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi
leo ili apitie hoja hizo na kuziandikia uamuzi na ndipo alipoamua kumuachia kwa
dhamana.
No comments