Header Ads

Kiongozi wa waasi ajisamilisha DR Congo



https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/13A9B/production/_97093508_ntabo.jpg

KINSHASA- MMOJA miongoni mwa wapiganaji wa vita maarufu nchini, Ntabo Ntaberi Sheka amejisalimisha kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Kikosi maalumu cha kulinda amani nchini, (MONUSCO), kimesema Sheka ndiye kiongozi mkuu wa kijeshi wa kundi lililokuwa likijulikana kama Mai-Mai Sheka, ambaye aliamua kujisalimisha karibu na ngome yake Mashariki mwa nchi.
Baada ya kujisalimisha, hatua inayofuata ni kukabidhiwa kwa Serikali ya nchi, ambayo miaka sita iliyopita ilitoa hati ya kukamatwa kwake kwa madai na makosa ya Uhalifu dhidi ya Binadamu na Uhalifu wa vita.
Kundi hilo la Mai-Mai Sheka, linatuhumiwa pia kwa makosa ya ubakaji na ukatili wa kutisha wa kuwatesa raia na na kuwaacha wafe taratibu.
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu lililoko mjini New York, limetoa rai kwa Serikali kumtendea mtuhumiwa huyo ubinadamu wakati wote wa kesi yake na kwamba haki zake kama binadamu zisikiukwe. 
BBC

No comments

Powered by Blogger.