Ikulu ya Marekani yadai azimio la kumng’oa Trump halina maana
Wabunge wawili wa chama Democratic, Al Green wa D-Texas na Brad Sherman wa D-California ambao wamewasilisha azimio la kulitaka bunge la Congress kumuondoa madarakani Rais Donald Trump.
WASHINGTON DC- IKULU ya Marekani, imesema azimio la kulitaka bunge kumuondoa
madarakani Rais, Donald Trump, ambalo limewasilishwa na wabunge wawili wa
Congress kutoka chama cha Democratic, halina maana.
Azimio hilo liliwasilishwa jana bungeni hapo na wabunge wawili ambao ni,
Al Green kutoka D-Texas na Brad Sherman kutoka D-California. Kwa pamoja, wabunge
hao wanataka bunge kutumia sheria iliyopitishwa mwaka 1974 inayohusiana na
kizuizi cha haki, ambao ulitumika kumuondoa Rais Richard Nixon.
Msemaji wa Ikulu, Sarah Huckabee Sanders alisema azimio hilo linadai
kwamba Trump alitumia mamlaka yake kuzuia uchunguzi na kusababisha kusitishwa kwa
uchunguzi wa madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa mwaka jana.
“Nafikiri kwa ujumla azimio hilo halina maana kabisa na ni mchezo wa
kisiasa ulio kwenye ubora wake mbaya,” Huckabee alisema wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari bila kuongeza maoni mengine.
abc NEWS
abc NEWS
No comments