Header Ads

Korea Kaskazini: Kombora letu la Hwasong 14 linafika Marekani



North Korean leader Kim Jong-un reacts during test launch in undated photo released by North Korea's Korean Central News Agency on May 15, 2017

PYONGYANG- SERIKALI imesema jaribio la kombora la masafa marefu, lililofanyika jana limeonesha mafanikio makubwa na pia limedhihirisha lina uwezo wa kufika Marekani.
Aidha, Serikali imeeleza kuwa mafanikio ya kombora hilo la Hwasong 14 lenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine (ICBM), ni onyo kwa taifa hilo la Amerika Kaskazini.
https://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/169BA/production/_97120629_mediaitem97116954.jpg
Kombora la Hwasong 14
Akizungumza mara baada ya tukio hilo, Rais Kim Jong-un alisema jaribio hilo la Hwasong 14 limethibitisha kuwa linaweza kupiga sehemu yoyote ya Marekani.
Ni wiki tatu ndizo zilizopita tangu kufanyika kwa jaribio la kombora lingine, lakini hili limeonesha mafanikio zaidi ya lile la Julai 3, mwaka huu ambalo nalo liliangukia sehemu ya bahari karibu na Japan.
Akithibitisha jaribio hilo, Rais Kim Jong-un alisema kombora hilo lilisafiri umbali wa kilometa 3,724 juu angani kwa muda wa dakika 47 pekee.
Katika kujibu mapigo, Korea Kusini na Marekani nazo zilifanya majaribio ya makombora maalum ambayo yalidondokea kwenye maji yaliyo kwenye umiliki wa taifa hilo la jirani.
Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini,Song Young-moo alisema wanaandaa njia huru za kudhibiti vitisho vya Korea Kaskazini na wataharakisha usimikaji wa mitambo ya kutungua makombora kutoka Marekani iitwayo THAAD.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.