Marekani kuziwekea vikwazo Urusi, Iran na Korea Kaskazini

WASHINGTON
DC- BARAZA la Wawakilishi la Marekani (Congress), limepiga kura ya kuidhinisha kuwekwa
kwa vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.
Urusi
inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana nchini,
huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiadhibiwa kufuatia majaribio ya makombora.
Muswada huo
unatarajiwa kupitia kwa Baraza la Seneti, kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili
auidhinishe na kuwa sheria kamili.
Akizungumza
katika baraza hilo, David Ciciline kutoka chama cha Democratic, alisema hatua
kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi.
Ciciline alisema
hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao
anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita.
Naye Ted Poe
kutoka chama cha Republican, alisisitiza kuwa muswada huo unaihusisha Korea Kaskazini
pia.
Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya Bunge la Urusi, (Duma),
Leonid Slutsky alisema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya Urusi na
Marekani.
BBC.
No comments