Tetesi za usajili; Man Utd kutoa £166m kwa Lukaku na Morata # PSG yatoa £ kwa Coutinho # Atletico Madrid yaweka £ 22m kwa Costa

LONDON- KLABU ya Manchester United wanakaribia kufanya
uhamisho wao mkubwa wa majira ya kiangazi, kutokana na timu hiyo kujiandaa kuipiku
Chelsea kwa kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton kwa dau la pauni milioni 100
(sh bilioni 290). Daily Mail

Gazeti la Marca la Hispania, linaripoti kuwa Man United wameweka
mezani kwa Real Madrid dau la pauni milioni 66 (sh bilioni 191.4) kwa ajili ya
kumsajili mshambuliaji Alvaro Morata (24).
PSG ya Ufaransa, wametangaza kuwa tayari kutoa dau la pauni milioni 70
(sh bilioni 203), kwa ajili ya kupata huduma ya kiungo wa Liverpool ya
Uingereza, Philippe Coutinho (25) ambaye msimu uliopita alitikisa nyavu mara
13. Daily Express.

Atletico Madrid wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 22 (sh bilioni 63.8)
ili kuipata tena huduma ya Diego Costa (28) ambaye anatarajiwa kuuzwa Chelsea
muda wowote. Guardian.

Kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier, amesema anaamini Arsenal
wanaweza wakawa wamempata ‘Ian Wright’ mpya baada ya kumnasa mshambuliaji,
Alexandre Lacazzette (26) kutoka Olympic Lyon. TalkSport.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez (28) amesema anataka mshahara wa
pauni 400,000 (sh bilioni 1.16) ili aweze kubakia klabuni hapo, ikiwa ni
ongezeko la pauni 125,000 (sh milioni 262.5) kutoka mshahara wake wa sasa. Daily
Miror.
West Ham United wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Burnley,
Andre Gray (26) kwa dau la pauni milioni 15 (sh bilioni 43.5). mchezaji huyo
amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake. Evening Standard.

Wageni wa Ligi Kuu, Huddersfield wako karibu kabisa kukamilisha usajili
wa mlinzi wa kati wa FC Copenhagen, Mathias Jorgensen kwa dau la pauni milioni
3.5 (sh bilioni 10). The Sun.

Kiungo wa Chelsea, Nathaniel Chalobah (22) anafanya mazungumzo na klabu
ya Watford kwa ajili ya kujiunga nayo kwa ada ya pauni milioni 5 (sh bilioni 14.5).
Daily Miror.
Asante kwa kuwa nasi na kwa heri hadi hapo jioni tena
No comments