Aishi bila kuwa na virusi vya Ukimwi licha ya kuzaliwa navyo
Mtoto
huyo, alipewa dawa za majaribio ya kukabiliana na virusi hivyo alipokuwa mdogo
lakini hakuwahi kupewa tena dawa zozote za kukabiliana na VVU tangu afikishe
umri wa mwaka mmoja.
Hii
ni mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa na virusi hivyo kuweza kuishi bila virusi
hivyo barani Afrika. Wanasayansi waliogundua kisa hicho, kwa sasa wanalinda
utambuzi wa mtoto huyo ambaye ana umri wa miaka 9 na nusu.
Wanasema
kuwa, visa kama hivyo ni vichache na kwamba familia ya mtoto hyo ina furaha. Dawa
hiyo alipewa mtoto huyo wakati ambapo haikuwa suala la kawaida.
Watafiti
wanaamini kupotea huko kwa vurusi siyo kwa sababu ya matibabu, lakini mtoto huyo
ana jeni ama kinga isiyokuwa ya kawaida ambazo zimemlinda dhidi ya VVU.
BBC
No comments