Jioni Leo; Morata apewa namba 9 # Mendy atua Man City # City watumia £200 # Neymar aikoroga Barcelona
LONDON- CHELSEA
imesema kuwa, mshambuliaji wao mpya kutoka Real Madrid, Alvaro Morata (24)
atavaa jezi namba 9 wakati kipa wao, Willy Caballero atavaa namba 1 huku
Antonio Rudiger akikabidhiwa namba 2 na kiungo Tiemoue Bakayoko atapatiwa namba
14. Sky Sports.
Beki
wa kushoto wa zamani wa Monaco, Benjamin Mendy, amesaini mkataba wa miaka
mitano wa kuichezea Manchester City kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 49.2
(sh bilioni 142.68) na kukabidhiwa jezi namba 22. Sky Sports.

Manchester
City inakuwa klabu ya kwanza kwa Uingereza, kutumia zaidi ya pauni milioni 200
(sh bilioni 580) kwa msimu mmoja kufanya usajili na kuweka rekodi. Sky Sports.
Hatima
ya mchezaji wa Brazil na Barcelona, Neymar, limeendelea kuikoroga Barcelona,
baada ya jana mchezaji mwenzie, Gerald Pique kuposti kwamba mshambuliaji huyo
haondoki lakini mtu wa karibu zaidi na Neymar amedai kuwa ataondoka. ESPN.

Southampton
imeweka wazi orodha ya wachezaji walio kwenye kikosi chake kilichopo kwenye ziara
za maandalizi ya kabla ya msimu, lakini kuna jina limekosekana nalo ni Virgil
van Dijk. Klabu hiyo imedai kuwa, kwa sasa Dijk amekuwa akifanya mazoezi peke
yake na anasisitiza anataka kuondoka klabuni hapo. Mail.
Winga
wa Leicester City, Riyad Mahrez (26) anaongoza orodha ya wachezaji wanaotakiwa
kwa udi na uvumba na Roma ya Italia, licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa miamba
hiyo inamuwinda pia mchezaji wa Manchester City, Samir Nasri (30). Leicester Mercury.
Mshambuliaji
wa Arsenal, Lucas Perez (28), amepewa ofay a mkataba mnono wa miaka 10 na klabu
ya Deportivo La Coruna, wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu hatima ya Mhispania
huyo pale Emirates Stadium. Metro.
No comments