Carzola kukosekana tena msimu ujao # Bellerin aomba kuondoka Arsenal # Mbappe ataka mshahara mnono Madrid

LONDON- KIUNGO wa Arsenal Santi Carzola, 32, ambaye
hajacheza tangu Oktoba 2016, huenda akakosa msimu ujao wote wa 2017/18 kutokana
na kuendelea kuwa majeruhi (Daily
Express).
Beki wa
Arsenal, Hector Bellerin, 22, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka,
lakini meneja Arsene Wenger amekataa ombi lake la kutaka kuondoka. Barcelona
wanataka kumsajili beki huyo kwa pauni milioni 35 (Daily Express).
Mshambuliaji
wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, ametoa sharti la kuwa mchezaji anayelipwa zaidi
nyuma ya Cristiano Ronaldo iwapo Real Madrid wanataka kumsajili (Diario Gol).

Meneja wa
Leicester City ametoa dau la pauni milioni 20 kumtaka mshambuliaji wa Watford,
Troy Deeney, 29 (Daily Mirror).

Juventus
wamempa beki wao Alex Sandro, 26, mshahara wa pauni 84,000 kwa wiki ili
kumshawishi asiondoke kwenda Chelsea ambao wapo tayari kutoa pauni milioni 61
kumnunua (London Evening Standard).
Tottenham
wanataka kumsajili Alfie Mawson, 23, kutoka Swansea, au Ben Gibson, 24, kutoka
Middlesbrough, huku wakitaka kumuuza beki wao wa kati Kevin Wimmer, 24 kwa
pauni milioni 20 (Daily Mirror).
Crystal
Palace wanafikiria kusajili mabeki wawili Joel Veltman, 25, na Kenny Tete, 21,
kutoka Ajax kwa pauni milioni 10 (Guardian).
Newcastle
wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26 (Shields Gazette).
No comments