Wataalam wagundua chanjo ya udukuzi


LONDON- WATAFITI wa usalama mitandaoni, wamegundua chanjo
ya shambulio la uhalifu wa mitandaoni lililoathiri mashirika tofauti duniani jana.
Utengenezaji
wa faili moja unaweza kuzuia shambulio la mashine yote. Hata hivyo, watafiti hao
hawajafanikiwa kupata suluhu ya mara moja itakayoweza kuzuia kirusi hicho
kuenea katika kompyuta nyingine ambazo hazina kinga.
Wataalam
bado hawajui shambulio hilo linatoka wapi na lengo lake ni nini.
Huku
ikidaiwa kwamba kikombozi inachotaka ni cha kiasi kidogo cha dola 300, wengi
wanadai kwamba shambulio hilo linaweza kusababisha madhara mabaya zaidi ama
hata kutoa tamko la kisiasa.

Baadhi ya
waathiriwa wa shambulio hilo ni Benki Kuu ya Ukraine, kampuni kubwa ya mafuta
kutoka Urusi, Rosnet, kampuni ya matangazo ya Uingereza, WPP na kampuni ya
mawakili wa Marekani, DLA Piper.
Pia,
waliopatikana katika shambulio hilo ni hospitali moja ya Marekani katika mji wa
Pittsburgh. Lakini kwa wale walio na wasiwasi kuhusu shambulio hilo, kunaonekana
kuna dawa inayoweza kudhibiti athari za kiini hicho.
Kwa
kutengeza faili kwa jina Perfc na kuiweka katika "C:\Windows" folder,
shambulio linaweza kusitishwa mara moja. Maelezo ya kufanya hivyo yamechapishwa katika
kompyuta ya usalama na kusaidiwa na wataalam wengine.
Hata hivyo,
huku mbinu hiyo ikiwa ina uwezo wa kudhibiti kirusi hicho, ina uwezo wa
kuzilinda kompyuta za kibinafsi ambazo faili zina Perfc. Watafiti kufikia sasa
wameshindwa kupata suluhu ya kudumu itakayozuia shambulio hilo kabisa.
Ijapokuwa
inaweza kuifanya mashine kuwa na kinga kama alivyoelezea mwanasayansi wa
kompyuta, Profesa Alan Woodward, bado inaweza kusambaza kiini hicho katika
kompyuta nyingine zilizounganishwa.
Kwa watumiaji
wengi, kuweka Windows mpya ni suluhu ya kuzuia shambulio hilo iwapo ingetaka
kuathiri komyuta yako.
Kusambaa kwa
kirusi hicho kipya, kunaweza kuwa kwa mwendo wa pole ikilinganishwa na kile cha
mwezi uliopita cha WannaCry na wataalam wametabiri huku wachangunuzi wa alama
za siri wakisema kuwa kirusi hicho hakikuwa na lengo la kusambaa zaidi ya lengo
lake.
Kutokana na
hilo, wataalam kadhaa wanatabiri kwamba shambulio hilo halitasambaa sana kama
lilivyofanya jana hadi pale kiini hicho kitakapoimarishwa.
No comments