Afa baada ya kumuokoa mwanae baharini

RIO VISTA,
California – MLINZI wa eneo la pwani
mjini hapa, amesema mwanaume mmoja ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40,
amepatikana akiwa amekufa baada ya kufanikiwa kumuokoa mwanae aliyezama
baharini.
Imeelezwa kuwa mwanaume huyo ambaye ametambulika kama Roni Avila,
alipotelea majini baada ya mwanae ambaye alikuwa ameambatana naye majini kwa boti
maalum kuokolewa na ndege maalum ya uokoaji.
Awali kabla ya ndege hiyo kufika eneo hilo, Avila alikuwa amefanikiwa
kumudu kumbeba bagani mwanae huyo mwenye umri wa miaka mitano baada ya kumuopa
majini kutokana na mtoto huyo kuangukia majini.
Inadaiwa kuwa chombo hicho walichokuwa wakikitumia, kilipinduka na
kusababisha mtoto huyo kuzama majini kabla ya kuokolewa na baba yake na kumbeba
begani hadi hapo ndege hiyo ilipomwokoa na kisha yeye kuzama majini na
kutoonekana hadi pale mwili wake ulipoonekana.
Kwa mujibu wa wachunguzi maalum na walinzi wa pwani, Avila na mwanae huyo
wa kike hawakuwa wamevaa maboya kwa ajili ya kuwanusuru kwenye kadhia za kuzama
baharini.
No comments