Kupanda kwa bei kukwamisha usajili wa Morata Man United

MANCHESTER- MPANGO wa klabu ya Manchester United
kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata, huenda ukakwama kutokana
na kupanda kwa bei ya mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, bei ya Morata
imepanda hadi kufikia pauni milioni 80 (sh bilioni 176) ikiwa ni ziada ya pauni
milioni 8 kutoka ile ya awali ya pauni milioni 72.
Hata hivyo, vyombo vingi vimeripoti kwamba mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 amekatisha fungate yake ili aweze kuharakisha
uhamisho wake kuelekea Man United.
No comments