Tetesi za usajili Ulaya leo

Manchester
City sasa wanaongoza katika mbio za kumsajili Alexis Sanchez (pichani), baada ya
Bayern Munich kujitoa kutokana na bei kubwa ya mchezaji huyo wa Arsenal (Daily
Mirror).
Manchester
City wana uhakika wa kumsajili Alexis Sanchez kwa takriban pauni milioni 50,
kwa sababu ya hamu ya mchezaji huyo kufunzwa na Pep Guardiola (Guardian)
Chelsea
wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris St-Germain katika kumsajili beki Alex
Sandro, 26, huku Juventus wakitaka pauni milioni 61 (Daily Mail).
Chelsea
wanatazamiwa kukamilisha usajili rasmi wa Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco wiki
hii (The Sun).
Wakala wa
kiungo wa Chelsea Mario Pasalic, wamekutana na Real Betis kujadili uhamisho wa
mchezaji huyo kwenda Spain (Marca).
Manchester
United watazidiwa kete na Paris St-Germain katika kumsajili kiungo kutoka
Brazil, Fabinho, 23 anayechezea Monaco (Daily Record).
Dau la
Arsenal la zaidi ya pauni milioni 30, la kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar,
21, limekataliwa, na sasa Arsenal wanafikiria kukamilisha usajili wa Riyad
Mahrez, 26, kutoka Leicester (Telegraph).
Barcelona,
Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomnyatia winga wa Monaco,
Thomas Leimar (L"Equipe).
Arsenal
wanamtaka kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 25, baada ya Roma kukatishwa tama
na bei ya pauni milioni 35 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast
(The Sun)
Mshambuliaji
wa Arsenal Olivier Giroud anakaribia kurejea Ufaransa, huku Lyon na Marseille
wakimtaka, na Arsenal ikitafuta mtu wa kuziba pengo lake (L'Equipe).

Chelsea
huenda wakatibua dau la Zenith St Petersburg la pauni milioni 26 la kumtaka
beki wa Roma, Kostas Minolas (pichani), huku mchezaji huyo pia akisita kuhamia Urusi
(Daily Telegraph).
Michel Keane
hatarajiwi kurejea Burnley kwa sababu Everton wanatarajiwa 'kulazimisha'
usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii (Burnley Express).
Michael
Keane atagharimu pauni milioni 25 (Times).
Mshambuliaji
wa Watford Stefano Okaka, 27, amepewa dau kubwa la kuhamia Shanghai Shenhua ya
China (The Sun).
Arsenal
wameambiwa lazima walipe pauni milioni 57 ili kumsajili Alexandre Lacazette,
26, kutoka Lyon (London Evening Standard).
Kinda wa
Arsenal Kaylen Hinds anajiandaa kuondoka Emirates na kujiunga na Wolfsburg ya
Ujerumani (The Sun).

Mshambuliaji
wa Real Madrid Gareth Bale (pichani) yuko tayari kuondoka Spain na kuhamia Manchester
United (Daily Star).
AC Milan
wanapanga kutoa kitita kikubwa kumsajili kiungo wa Real Madrid Isco (Don
Balon).
AC Milan
wanakaribia kumsajili Hakan Calhanoglu kutoka Bayer Leverkusen kwa euro milioni
20 (Sky Sport Italia).
West Brom
wanakaribikia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez,
27 kwa pauni milioni 12 (Daily Express).
Nahodha wa
zamani wa Chelsea John Terry, 36, ameambiwa anaweza kuchukua nafasi ya umeneja
wa Aston Villa, iwapo atajiunga na klabu hiyo (Daily Express).
Mchezaji
anayenyatiwa na Liverpool Naby Keita, 22, amesema angependa kuchezea moja ya
timu kubwa kama vile Barcelona, Real Madrid au Manchester City. Liverpool
wanamtaka kiungo huyo wa Red Bull Leipzig (Manchester Evening News).

Beki wa
Chelsea Nathan Ake, 22 (pichani), anakaribia kufanikisha uhamisho wake wa pauni milioni
20 kwenda Bournmouth (Guardian).
Pierre
Emerick-Aubameyang, 28, anayenyatiwa na Liverpool anaonekana kukaribia
kukamilisha uhamisho wake kwenda Tianjin Quanjian ya China, ambayo imetoa dau
la pauni milioni 70 (Daily Star).
Real Madrid
bado wanafikiria kuhusu Kylian Mbappe, kwa mujibu wa Rais wa Real, Florentini
Perez, ambaye anasema umri wake wa miaka 18 huenda ukawa tatizo katika klabu
hiyo ingawa amekiri kuwa Zinedine Zidane yuko karibu na mchezaji huyo na
usajili unaweza kufanyika (Independent).
Winga wa
Everton Gerard Deulofeu, 23, amekataa nafasi ya kurejea Barcelona, huku AC
Milan na Juventus pia zikimtaka (Daily Mail).
Newcastle
United wanazungumza na Liverpool kuhusu uhamisho wa mkopo wa winga Sheyi Ojo,
20 (Newcastle Chronicle).
Mkurugenzi
mkuu wa Southampton Les Reed amesisitiza kuwa mabeki wake Virgil van Dijk na
Cedric Soares hawauzwi. Liverpool na Tottenham zinawataka wachezaji wao (Sky
Sports).

Leicester
City hawajapokea dau lolote la kumtaka Riyad Mahrez (pichani), ambaye amehusishwa na
kuhamia Arsenal, Barcelona na Chelsea (Leicester Mercury).
Juventus
wanafikiria kumchukua beki wa Real Madrid Danilo, kuziba nafasi ya Dani Alves
anayetazamiwa kwenda Manchester City (Corriere dello Sport).
Habari
zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya
wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii:
http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
No comments