Makosa matano ambayo wanatuhumiwa Rais wa Simba na Makamu wake
Alhamisi ya
June 29 2017 Rais wa club ya Simba Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange
Kaburu walifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam kusikiliza
mashitaka yao.
Evans Aveva
na Kaburu wameshtakiwa kwa makosa kwa matano ambayo kwa mujibu ya sheria
yanawanyima dhamana hivyo wamelazimika kwenda lumande hadi July 13 ndio
kesi yao itaendelea chini hakimu Victoria Nongwa.
Kutoka kulia ni Rais wa Simba Evans Aveva na wa
pili kulia ni makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'
Makosa matano wanayotuhumiwa nayo viongozi wa Simba
1- March 5 2016 Evans Aveva anatuhumiwa kugushi
nyaraka za kuidai Simba dola 300,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh
milioni 600.
2-March 16 zilitumika nyaraka za uongo kujilipa
deni kupitia bank ya CRDB Azikiwe.
3- Kula njama na kutakatisha fedha kinyume cha
sheria kiasi cha dola 300,000 za kimarekani.
4- Kosa la nne Evans Aveva anatuhumiwa kutakatisha
fedha ambazo alizipokea kupitia bank ya Barclays tawi la Mikocheni.
5- Kaburu anatuhumiwa pia kumsaidia Evans Aveva
kutakatisha fedha dola za kimarekani 300000 kupitia Bank ya Barclays tawi la
Mikocheni.
Makamu wa Rais wa Simba Kaburu mwenye shati jekundu akiongea na wakili
Kwa mujibu wa sheria makosa ya kutakatisha fedha
hayana dhamana hivyo Rais wa Simba Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange
Kaburu watakuwa lumande hadi July 13.
Chanzo; Millard Ayo
No comments