Header Ads

Shambulizi la Manchester lilipangwa tangu Desemba mwaka jana



Salman Abedi na gari lake kulia wakati akijiandaa kwa shambulizi hilo
Mshambuliaji wa Manchester, Salman Abeid katika picha mbili za tofauti. Kushoto akijiandaa kuondoka kwake na kulia ni gari alilotumia kuelekea ukumbini siku ya tukio.
TRIPOLI- MAOFISA usalama wa Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini, wameiambia BBC kuwa shambulizi la mjini Manchester, Uingereza lilipangwa tangu Desemba mwaka jana.

Wanasema kuwa mshambuliaji Salman Abedi, alikua akifuatiliwa nyendo zake na wanausalama wa Libya kabla ya kusafiri kuelekea Uingereza kufanya shambulizi hilo.
Mmoja wa kaka yake (Hashem) na baba yake (Ramadan), pia walikuwa wakifuatiliwa na kwa sasa wanashikiliwa na polisi. Haijawekwa wazi iwapo maofisa wa Libya walitoa taarifa kwa wale wa Uingereza.

No comments

Powered by Blogger.