Kiongozi wa upinzani Urusi atupwa jela

MOSCOW- KIONGOZI wa upinzani nchini, Alexei Navalny
amehukumiwa kifungo cha siku 30 jela kwa kukiuka sheria baada ya kuandaa
maandamano.
Navalny (pichani) alikamatwa
nyumbani kwake mjini hapa jana, kabla ya kufanyika kwa maandamano ya kupinga
ufisadi nchini. Mamia ya watu walikamatwa wakati wa maandamano hayo
yaliyofanyika kote nchini.
Polisi wa
kupambana na maandamano, walikuwa wakiwakamata waandamanaji kutoka kwa umati,
kwa mujibu wa mwandjshi wa BBC aliyekuweko.
Mahakama ilitangaza
umuzi wake jana, na kukataa wito wa mawakili wa Navalny kufuta kesi hiyo. Kiongozi
huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 42, baadaye alithibitisha hukumu yake
katika mtandao wa Twitter.
Polisi mjini
hapa wanasema kuwa takriban watu 5000 walishiriki maandamano hayo.
No comments