Meli za Oman kupeleka chakula Qatar

Baadhi ya makontena yenye chakula kutoka Oman, yakipakiwa kwenye meli kwa ajili ya kupelekwa Qatar.
DOHA- SERIKALI imefungua mpaka wake na Oman, kwa ajili
ya kuruhusu huduma za usafiri wa meli kutoka nchini humo kwa lengo la
kukabiliana na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na majirani.
Meli kadhaa
zikiwa zimebeba vyakula na bidhaa mbalimbali, zimeonekana zikichukua uelekea wa
kuja nchini kutokea bandari mbili zilizopo nchini humo. Qatar inategemea kwa
asilimia kubwa uingizwaji wa chakula kutoka nje.
Saudi
Arabia, Bahrain na Muungano wa Falme za Kiarabu, zilizuia uingizwaji wa bidhaa nchini
wiki chache zilizopita kwa shutuma kuwa Qatar inaunga mkono vitendo vya
kigaidi.
Waziri wa Mambo
ya Nje nchini amewasili mjini London na kisha Paris kujadili mgogoro huo. Wakati
hatua ya kuitenga Qatar ilianza wiki iliyopita, kulikuwa na ripoti za watu
kununua chakula kwa wingi wakihofia kuwepo upungufu.
Lakini
mwishoni mwa wiki, bidhaa kutoka Uturuki zilianza kuwasili katika maduka na
ndege tano zilizosheheni matunda na mboga nazo ziliondoka nchini Iran. Meli
tatu zilizosheheni tani 350 za chakula pia zinatarajiwa kuondoka nchini Iran
kuelekea nchini.
Waziri wa
Mambo ya Nje anasema kuwa asilimia 16 ya chakula chake kilikuwa kinasafirishwa
kupitia Saudi Arabia ambayo ilifunga mpaka wake.
No comments