Header Ads

Pacquiao mbioni kuzichapa na Mayweather tena



BRISBANE- LEGENDARI wa ngumi wa Kifilipino, Manny Pacquiao anakaribia kutimiza ndoto zake za kurudiana tena na Mmarekani, Floyd Mayweather, iwapo tu atafanikiwa kushinda pambano lake dhidi ya bondia wa Australia, Jeff Horn.

Pambano hilo ambalo litafanyika mjini hapa mnamo Jumapili Julai 2, mwaka huu, linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na rekodi nzuri ya mpinzani huyo wa Pacquiao ambaye hakuwahi kupoteza pambano lolote.
Ili kunogesha pambano hilo zaidi, kambi ya Mfilipino huyo aliye chini ya kocha Freddie Roach, tayari imeeleza kwamba imeshafanya mazungumzo na kambi ya Mayweather na ushindi wa Pacquiao ambaye anatakiwa ashinde kwa KO, utaharakisha kukamilika kwa marudiano ya mabondia hao.
“Tunafukuzia pambano la marudiano na Mayweather na tunajua kuwa (Pacquiao) akishinda kwa KO, itakuwa fursa nzuri ya kufanikisha pambano hilo la marudiano. Ushindi kwenye pambano hili, itakuwa kitu kizuri zaidi,”
“Nafahamu kwamba atashinda pambano hilo tena kwa KO, kitu ambacho nimekuwa nikikisubiri kwa muda mrefu na natarajia kitatokea siku hiyo,” alisema kocha Roach.
Hata hivo, pambano hilo linatarajiwa kuwa gumu zaidi kutokana na rekodi nzuri aliyonayo Horn ambaye ana taaluma ya ualimu.
Courier Mail

No comments

Powered by Blogger.