Header Ads

Trump kukutana na Putin wiki ijayo



Trump na Putin walikubaliana kufanya kazi pamoja siku za nyuma
WASHINGTON DC- IKULU ya Marekani (White House), imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin wiki ijayo, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20).

Utakuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baina ya viongozi hawa wawili. Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani, H.R. MacMaster amesema bado hakuna mada maalumu iliyopendekezwa.
Mapema msemaji wa ikulu ya Kremlin alithibitisha uwepo wa mkutano huo.
BBC

No comments

Powered by Blogger.