Header Ads

Mwanamke amuua mpenziwe kwa mzaha wa YouTube



Amuua mpenziwe kwa ''mzaha'' katika YouTube
MINESOTTA- MWANAMKE mmoja mjini hapa, amekamatwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake katika kile kinachosemekana ni mgogoro wa mtandaoni.

Monalisa Perez mwenye umri wa miaka 19, amewekwa kizuizini baada ya kumpiga risasi Pedro Ruiz alipokuwa akishikilia kitabu katika kifua chake akidhani kitazuia risasi hiyo.
Wawili hao wana mtoto wa miaka mitatu na takriban watu 30 walikuwa wakiangalia video hiyo ya YouTube alipompiga risasi mpenziwe.
Shangazi yake Ruiz anasema kuwa, walifanya kitendo hicho ili kuimarisha ufuasi wao katika katika mitandao ya kijamii.
Claudia Ruiz aliambia runinga ya WDAY-TV kwamba binamu yake alimwambia kwamba alitaka kufanya kitendo hicho ‘kwa sababu walihitaji kupata wafuasi zaidi, na kuongeza kuwa walidai ‘tunataka kuwa maarufu’.
“Aliniambia kuhusu wazo hilo na nikamwambia, ‘Musafanye hivyo’. Kwa nini utumie bunduki? Kwa nini?” Claudia Ruiz alikiambia chombo hicho cha habari.
“Walikuwa wakipendana sana. Ulikuwa mzaha uliofanyika kimakosa” alisema Claudia Ruiz.

No comments

Powered by Blogger.