Afungua kesi mahakamani kutaka Raila Odinga azuiliwe kugombea urais Kenya

NAIROBI- MTU
mmoja jijini hapa, amefungua shauri mahakamani ambalo linataka mgombea urais
kupitia Muungano wa Vyama vya Upinzani Kenya (NASA), Raila Odinga kuzuiwa
kuwania nafasi hiyo Agosti 8 mwaka huu.
Shauri hilo
liliwasilishwa mahakamani na Charles Ndungu Mwangi, ambaye ameitaka mahakama
kumtaka Waziri wa Elimu nchini, Dk Fred Matiang’i kuwasilisha mahakamani hapo
vyeti vya elimu vya shule ya msingi, sekondari na kile cha shahada ya uhandisi
cha kiongozi huyo.
“Kiongozi wa
upinzani hayuko juu ya Katiba na sheria ya Kenya na anapaswa kuiheshimu,
kuitunza na kuilinda na kushindwa kufanya hivyo kutasababisha yeye ajaribu
kutengeneza Serikali isiyo halali,” alidai mlalamikaji.
Katika shauri
hilo, mlalamikaji amewajumuisha pia Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini
(IEBC), Wafula Chebukati; Mwenyekiti wa EACC, Eliud Wabukala; Mkuu wa Jeshi la
Polisi, Joseph Boinett; Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Elimu.
Mlalamikaji huyo
alidai kuwa Waziri wa Elimu ameshindwa kutoa kwa umma taarifa kamili za elimu
ya Raila.
No comments