Jengo la ghorofa 7 laporomoka Nairobi

NAIROBI-
WATU zaidi ya 15 hawajulikani walipo, baada ya jengo la ghorofa 7 kuporomoka
ghafla usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kware Pipeline Embakasi, jijini hapa.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini, kupitia akaunti
yao ya Twitter, kikosi kazi cha uokozi cha shirika hilo tayari kipo eneo la
tukio kwa ajili ya shughuli za uokozi.
Taarifa nyingine
ya gazeti la Star, ilieleza kwamba watu wengi wameokolewa kutoka kwenye jengo
hilo.
BBC
No comments