Amri ya Trump yagonga mwamba tena

WASHINGTON
DC - MAHAKAMA ya Rufaa nchini, imemua kuwa uamuzi wa kuzuia mpango uliofanyiwa
marekebisho wa marufuku ya Rais Donald Trump, kuzuia watu kutoka nchi sita za Kiislamu
haistahili kuwepo.
Wakitoa
hukumu kufuatia kesi iliyowasilishwa na jimbo la Hawaii, majaji walieleza kuwa
amri hiyo kuu inakiuka sheria zilizopo za uhamiaji.
Rufaa hiyo
iliyowasilishwa katika Mahakama ya Rufaa ya San Fransisco, ni kufuatia umamuzi
uliotolewa kupinga raia ambao wengi wao wakiwa wa nchi za Kiislam kuingia
Marekani.
Hata hivyo,
mahakama haikusema kuwa Serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi
kwa watu wanaoingia nchini.
Msemaji wa
Ikulu, Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa Rais Trump, akisistiza kuwa kila
lilalowezekana linatakiwa kufanywa kwa ajili ya ulinzi wa Marekani
“Nadhan wote
tunafahamu kuwa hizi ni nyakati za hatari dhidi ya tishio la ugaidi, tunapaswa kulinda
kuingia kwa watu wanaoweza kufanya vitendo vya ugaidi na umwagaji damu. Tunaendelea
kuwa na imani kwamba, amri za rais wetu ni kwa mujibu sheria na kwamba
tunaamini mahakama ya juu itazipitisha,” alisema Spicer.
Hata hivyo, Mwanasheria
Mkuu wa jimbo la Maryland na Columbia, Brian Frosh amefungua mashitaka dhidi ya
Rais Trump kwa madai ya kupokea malipo ya nje kupitia makampuni yake.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa, Frosh ambaye anatokea kampuni ya Maryland's
Attorney Generel, aliseama Trump kujihusisha biashara akiwa madarakani ni
kuvunja katiba
“Aliiteuwa hoteli
yake ya kimataifa ya Trump kwaajili ya wanadiplomasia na maofisa wa Serikali.
Amekuwa akionekana kwenye sehemu nyingi za biashara zake na imekuwa kama sehemu
ya kutangaza biashara hizo.
Analipwa na
makampuni yanayo milikiwa na nchi za nje kama vile China, ambao pia ni
wapangaji katika majengo yake. Na amekuwa akiendelea kuchukua malipo kutoka
nchi za Saudi Arabia, India, Afghanistan na Qatar nchi ambazo zina hisa majengo
yake ya kibiashara yajulikanayo kama Trump World Tower,” alisema Frosh.
Rais Trump amekuwa akikabiliwa na
upinzani mkali, kufuatia baadhi ya maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya tangu
kuingia madarakani, ikiwemo hatua hii aliyoichukua kupiga marufuku raia kutoka
baadhi ya nchi za Kiislam kuingia Marekani.
No comments