IGP Sirro atembelea na kuzungumza na wanakijiji wa Mangwi, Kibiti
KIBITI- Siku moja baada ya kuripotiwa mauaji ya Mwenyekiti
wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi
wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea kijijini hapo
kutoa pole kwa wafiwa.
IGP Sirro akisalimiana na wakazi wa kijiji hicho
mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
Aidha, IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.
IGP Simon Sirro akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mangwi, Kata ya Mchukwi alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji.
IGP Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi
wa kijiji hicho alipowatembelea baada ya mauaji ya Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho.
IGP Sirro akizungumza na wakazi wa kijiji hicho
mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
Chanzo; Jamii Forum
No comments