Barcelona kukipiga na Chapecoense Agosti 7
BARCELONA- UNAIKUMBUKA ile timu ya Chapecoense? Ngoja
nikujuze kidogo, ni ile timu iliyopata ajali na kupoteza wachezaji wake 19 kwenye
ajali ya ndege iliyotokea huko Medellin nchini Colombia.
Iko hivi,
baada ya kuanza kushiriki tena ligi kuu ya kwao Brazil, sasa imepata mwaliko
rasmi wa kucheza na timu ya Barcelona ya Hispania mnamo Agosti 7 mwaka huu
kwenye dimba la Nou Camp.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Barcelona, mchezo huo unalenga kuirudishia
morali timu na kuiwezesha kurejea kwenye levo za kimataifa za ushindani.
Mshindi wa
mpambano huo, atatunikiwa tuzo maalum ambayo ni kombe la Joan Gamper.
No comments