Daktari atuhumiwa kupandikiza mbegu zake kwa wanawake Uholanzi
Daktari
huyo, Jan Karbaat anashukiwa kuwa baba wa watoto wapatao 60, katika kituo cha
afya alichomiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.
Vipimo
sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada
ya kifo chake Aprili mwaka huu, akiwa na umri wa miaka 89.
Wakili
wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo. Jan Karbaat
alijiita ‘muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa’.
Kliniki
yake ilifungwa mwaka 2009, wakati kulipokuwa na taarifa kwamba alidaiwa kugushi
data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiume na kuzidisha idadi
inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za
uzazi.
Katika
kesi mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba
visa vinavyoshukiwa vinajumuisha mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi
wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wakebambaye anasura
inayofanana na daktari.
Taarifa
za DNA zitasalia kuwa siri hadi pale watoto watakapoonesha kuwa kuna sababu za
kuamini daktari alikuwa baba yao, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan,
ambaye alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Rotterdam.
Hatimaye,
kama taarifa za DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya
1980, kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba
hawangepaswa kuwepo.
Joey,
ambaye anaamini Jan Karbaat huenda ni baba yake aliiambia BBC: “Ina maana kubwa
kwangu ... Tunatumai kupata majibu.”
Wakili
wa familia ya Karbaat anapinga kufanyika kwa vipimo vyovyote vya vinasaba DNA. Wakati
wa uhai wake, daktari mwenyewe alikataa kufanya vipimo hivyo.
Hata
hivyo, mwezi uliopita, mtoto wa Karbaat alitoa vinasaba vyake ili vipimwe ambavyo
vilionesha kuwa baba yake anaweza kuwa baba wa watoto 19, waliozaliwa kwa njia
ya uzazi wa kutungishwa mbegu kwa lugha ya kitaaamu IVF, kulingana na ripoti ya
shirika la habari la AFP.
No comments