Mwanafunzi Mwingereza asimulia maisha yalivyo Korea Kaskazini

Benjamin
Griffin akijumuika na wenzake kupata ‘kikombe cha chai’ katika jumba la urafiki
wa kimataifa nchini Korea Kaskazini.
LONDON,
Uingereza
KOREA Kaskazini
inapotajwa, linalotokea akilini mwa watu wengi huwa ni ubabe wa taifa hilo na majaribio
ya makombora na silaha za nyuklia, pamoja na kiongozi wake, Kim Jong-un.
Aidha, mara
kwa mara taarifa za raia wa nchi za Magharibi kukamatwa na kufungwa jela
huripotiwa. Lakini sasa kuna mwanafunzi Mwingereza, ambaye anaamini wengi
hawajalifahamu vema taifa hilo.
Badala ya
kuitenga Korea Kaskazini, anaamini wakati umefika kwa watu kufanya urafiki na
taifa hilo.
“Tumekuwa
wepesi wa kuibandika Korea Kaskazini maneno kama vile ‘marufuku’, ‘taifa lenye
usiri mkubwa’, ‘dhiki’, 'ukatili’ na kadhalika, lakini nataka kuondoa dhana
hiyo, angalau kwa dakika moja, tuitazame Korea Kaskazini katika ngazi ya utu,”
anasema Benjamin Griffin, mwenye umri wa miaka 24.
Kabla yake
kufanya ziara yake ya kwanza nchini humo miaka minne iliyopita, ufahamu wake
kuhusu nchi hiyo anasema ulitokana na ‘makala moja pekee aliyokuwa ameitazama
na video fupi za YouTube.’
Lakini alipata
nafasi ya kusafiri taifa hilo kwa kutumia shirika lakitalii la Juche Travel
Services (JTS), safari iliyomfumbua macho.

Benjamin (mwenye tai ya bluu) akiwa na wanafunzi wa utalii ambao anawafundisha nchini Korea Kaskazini.
“Nilipoiona
Pyongyang kwa mara ya kwanza mwaka 2013, nilitarajia kuwaona wanajeshi kila
nilikoenda. Ni kana kwamba sikuwa nawatazama kama watu halisi,”
“Lakini
ukweli ni kwamba tuliwaona watu wakitembea kwenda kazini, kwenda madukani na
kucheza ngoma katika bustani. Kwa kiasi fulani, nilishangazwa na maisha hayo ya
kawaida.
“Ukweli ni
kwamba, katika maisha ya kila siku ya raia wa Pyongyang, huwa hawana wasiwasi
kuhusu njia gani bora ya kukabiliana na ubabe wa Marekani au maovu ya mfumo wa
ubepari. Wanachokijali zaidi ni, 'Nitaenda wapi dukani kununua bidhaa?
Nimefikia wapi katika kazi yangu? Binti yangu ataolewa?” anasema Benjamin.
Mwaka
uliofuata, akiwa na miaka 21, alirejea huko kama mwalimu wa kujitolea wa somo
la Kiingereza katika chuo cha utalii cha Pyongyang.
Baadaye,
alihitimu na kuwa mwelekezi wa watalii wa TJS na sasa ameanzisha mpango wa
kuwasaidia watu wa kila tabaka au asili wanaotaka kwenda kukaa chuo kikuu cha Kim
Il-sung, Julai mwaka huu.
Washiriki
watalala katika mabweni ya chuo na kujifunza Kikorea kwa masaa manne kila siku.
Muda huo
mwingine watautumia kwa kutembea, kujionea mji na vivutio mbalimbali, na kisha
kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile kuogelea, kucheza ngoma asili na
kucheza mchezo wa kandadna wa wachezaji watano kila upande.
Aidha, kutakua
pia na fursa ya kukutana na baadhi ya raia wa Korea Kaskazini, ingawa raia hao
watakua wamechunguzwa kikamilifu.
“Hatuwezi
kamwe kusahau matatizo yaliyopo Korea Kaskazini, lakini tunafaa kua na uelewa
fulani. Utalii wa elimu unasaidia hilo. Sitaki kuacha kuuliza maswali, lakini
ni muhimu pia kuifahamu nchi hiyo kikamilifu, watu wake na thamani na maadili
yao.
“Ni kweli
kuna siasa - wana majaribio yao ya silaha za nyuklia, na ukiukwaji wa haki za
kibinadamu - lakini ni muhimu kuangazia uhusiano wa binadamu mmoja na mwingine.”
Anasema Benjamin.

Benjamin akifundisha wanafunzi somo la Kingereza katika Chuo Kikuu cha Utalii nchini Korea Kaskazini.

Benjamin
Griffin akiwa mbele ya kaburi la Kim II-sung nchini Korea Kaskazini.
No comments