Jinping awasili Hong Kong kuadhimisha miaka 20 ya utawala wa China
HONG KONG- LICHA
ya harakati mbalimbali za kudai uhuru kamili wa Hong Kong kutoka China, Rais Xi
Jinping amewasili mjini hapa ili kuadhimisha miaka 20 tangu China
ilipokabidhiwa utawala kamili juu ya Hong Kong.
Akizungumza mbele
ya halaiki iliyojitokeza uwanja wa ndege kumlaki, Rais Jinping alisema kwamba; “Baada
ya miaka 9, hatimaye tena naikanyaga ardhi ya Hong Kong. Ninajisikia furaha
isiyo na kifani, kwani Hong Kong imekuwa na sehemu kwenye moyo wangu muda wote.”
Hata hivyo,
ujio wa Rais Jinping mjini hapa haukufurahiwa na watu wote kwani kabla ya ujio
huo mamia ya wanaharakati na waandamanaji ambao wamekuwa wakidai uhuru kamili
wa Hong Kong wamekamatwa na kuwekwa ndani ili wasivuruge sherehe hizo
zinazotarajiwa kufanyika Jumamosi.
Miaka 20
iliyopita, utawala wa Uingereza uliirudisha Hong Kong katika mikono ya China
chini ya mfumo ujulikanao kama ‘Taifa moja, Mifumo miwili’ ambao unaipa mamlaka
China ya kuitawala Hong Kong kiuchumi na kiutawala.
SkyNews
No comments