Header Ads

WHO kukabiliana na mlipuko wa Ebola DRC



Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza mwaka 1976
Wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa kupambana na Ebola, wakiwa kazini.
GENEVA, Uswisi
SHIRIKA la Afya Duniani, WHO limeahidi kuchukua hatua za tahadhari za haraka zaidi, ili kuzima mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola ambao umetokea katika maeneo ya Kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO, wataalamu wa kiufundi wa shirika hilo wametumwa hadi maeneo ya vijijini, kunakoaminika kutokea visa 11 vya ugonjwa wa Ebola zikiwemo ripoti ya vifo vya watu watatu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa wataalam hao wanafanya kila mbinu kubaini upana wa mlipuko wa ugonjwa huo, kuwapa tiba walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo, na kuwatambua walioambukizwa au watu waliokaribiana na walioambukizwa virusi hivyo.
Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini DRC, tangu kisa cha kwanza cha Ebola kutambuliwa nchini humo mnamo mwaka wa 1976.

No comments

Powered by Blogger.