Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora masafa marefu

Magari ya kivita yakiwa na makombora ya masafa marefu yalipokuwa yakioneshwa siku ya maonesho ya kijeshi hivi karibuni nchini Korea Kaskazini. Makombora hayo yamefanyiwa majaribio na kuibua shutuma kote duniani.
SEOUL, Korea
Kusini
WAKATI
Mjumbe Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui
akisema kuwa endapo mazingira yakiruhusu watazungumza na Marekani, taifa hilo
limefanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Hatua hiyo
ya kufanya majaribio ya makombora hayo na zana za nyuklia, imeibua shutuma nyingi
kote duniani kulaani majaribio hayo yenye lengo la kuendelea kuleta hali ya
wasiwasi.
Marekani imetaka
vikwazo zaidi viongezewe kwa taifa hilo, huku Ikulu ya White House ikisema
kuwa, Korea Kaskazini imeachwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu.
Rais mpya wa
Korea Kusini, Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini cha
kufanya majaribio zaidi zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama kitendo cha
uchochezi.
Jeshi la
Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa karibu
na mji wa Kaskazini Magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya Japan.
Moon ambaye
alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Korea Kaskazini, wakati wa
kampeni zake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri
wake wa kiusalama.
Jaribio
lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba
wiki mbili zilizopita. Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa
pamoja na vikwazo na kufanya majaribio matano ya zana zake za masafa marefu za
nuklia.
No comments