Header Ads

Aamua kujioa kutimiza ndoto zake



Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa
TAIPEI, Taiwan
MWANAMKE mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti, amefikia uamuzi wa kujioa mwenyewe baada ya kusubiri kupata mchumba kwa muda mrefu.

May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan, aliiambia BBC kwamba anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
Q May Chen mwanamke mwenye saratni ya matiti aliyejioa
“Nimekuwa nikisubiri mtu (mwanaume) ajitokeze na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami, mbali na kupiga picha za harusi nami,” Chen aliiambia BBC.
Alisema kwamba, wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia masuala muhimu ili kutimiza ndoto zako. Anasema kwamba aliamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.
Chen anadai kuwa wapiga picha walimshauri kupiga picha katika studio, lakini yeye akawaambia kwamba anataka picha zilizo sawa na zile za harusi. Alisema aliamua kukodisha gari na kwenda kupiga picha hizo katika maandhari ya harusi.
“Nilipovalia rinda la harusi nilijawa na hisia mpaka nikahisi kulia. Nilihisi kana kwamba nimeafikia ndoto yake ya miaka mingi,” alisema Chen.
Kutokana na kuugua saratani ya matiti, Chen hulazimika kwenda hospitali mara tatu kwa wiki ili kudungwa sindano mbali na kutibiwa kwa kutumia kemikali.
Chen anabainisha kwamba, kwa muda mrefu hakuweza kusimama kwa miguu miwili na kuvaa suruali ndefu, kutokana na kulazimika kutembea kwa kutumia kiti cha magurudumu.
Anasema kwamba hakuweza kutembea na kwamba nywele alizo nazo sio nywele zake asilia. Habari ya mwanamke huo imewagusa watu wengi ulimwenguni.
Q May Chen mwanamke mwenye saratni ya matiti aliyejioa

No comments

Powered by Blogger.