Watu 19 wauawa kwenye mlipuko mjini Manchester
Polisi nchini, wamesema
watu wasiopungua 19 wameuawa na wengine 59 kujeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea
mwishoni mwa tamasha la muziki la mwanamuziki wa Marekani, Ariana Grande mjini hapa.
Polisi
na kikozi maalum cha uokozi jijini Manchester, Uingereza wakimsaidia majeruhi
wa mlipuko uliotokea jana na kuua watu 19 jijini humo kwenye tamasha la Ariana
Grande.
Maofisa wawili wa
Marekani walisema mshambuliaji wa kujitoa muhanga anashukiwa kuhusika na
mlipuko huo.
Waziri Mkuu, Theresa
May alisema tukio hilo linachukuliwa kuwa la kigaidi. May anatarajiwa kuongoza
kikao cha dharura cha kamati ya usalama kuanzia saa tatu asubuhi.
Vyombo kadhaa vya
habari vimeripoti kwamba kulitokea milipuko miwili ndani ya ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 21,000 waliokaa. Polisi wa Manchester walisema wanashirikiana na
polisi taifa na mashirika ya kijasusi kuchunguza mlipuko huo.
Meya wa mji wa London,
Sadiq Khan ametuma risala zake za rambirambi kwa jamii za wahanga na amesema
mji wa London unasimama pamoja na mji wa Manchester kufuatilia tukio hilo.
BBC
No comments