Muwindaji afariki kwa kuangukiwa na tembo Zimbabwe
HARARE,
Zimbabwe
MUWINDAJI
mbobezi wa wanyama, Theunis Botha amefariki dunia baada ya kuangukiwa na tembo
ambaye alipigwa risasi na wawindaji.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na wavuti ya Netwerk24, Botha alipoteza maisha wakati
alipoangukiwa na tembo jike aliyepigwa risasi na timu ya wawindaji waliokuwa
wakiongozwa na muwindaji huyo katika eneo la mbuga ya wanyama ya Hwange nchini
hapa.
Botha (pichani)
mwenye umri wa miaka 51, na baba wa watoto watano kutoka jimbo la Limpopo
nchini Afrika Kusini, alifikwa na mkasa huo wakati tembo huyo alipovamia eneo
walilokuwa wamepumzika wawindaji wengine akiwemo yeye.
Mara baada ya
tembo huyo kufika hapo, alianguka na kumwangukia Botha kabla ya kufa. Taarifa
hiyo inaeleza kwamba wawindaji wenzake na Botha, walijaribu kumwinua lakini
walikuta mwenzao tayari ameshapoteza maisha.
No comments