Wapenzi wa jinsia moja wachapwa viboko 85 Indonesia
ACHEH,
Indonesia
WANAUME
wawili wamechapwa viboko 85 kila mmoja mkoani hapa, baada ya kufumamwa
wakifanya mapenzi.
Wanaume hao
walisimama kwenye jukwaa wakiwa na mavazi meupe wakiomba, huku kundi la wanaume
likiwachapa vikobo kwenye migongo yao. Serikali imeharamisha mapenzi ya Jinsia
moja na mkoa huu hutawaliwa na sheria ya kidini- Sharia.
Adhabu hiyo
ilitolewa mbele ya umma. Wanaume hao wa
miaka 20 na 23 walifumaniwa wakiwa ndani kitandani na makundi ya sungusungu
yaliyovamia makazi yao Machi mwaka huu.
Kabla
ya kufumaniwa na kundi la sungu sungu, mmoja wao alikuwa ni mwanafunzi wa chuo
kikuu akisomea udaktari. Aliwaambia waandishi wa habari kuwa mipango yake
ilikuwa ni kuwa daktari. Kwa sasa inaripotiwa kuwa chuo kimemtimua mwanafunzi
huyo.
Video za
wawili hao wakifumaniwa, zilisambazwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii
wakiwa wote uchi huku wakiomba msaada. Sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia
moja zilipitishwa mwaka 2014 na kuanza kutekelezwa mwaka uliofuatia.
Hukumu za
kuchapwa viboko zilitolewa awali kwa makosa yanayohusu kucheza kamari na
unywaji pombe.
BBC
No comments