BASATA: Tunamtafuta Ben Pol atueleze kuhusu picha zake za utupu
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza amelaani picha
za nusu za utupu za msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Benard Paul (Ben Pol)
ambazo zimezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea
na Bongo5 jana, Mngereza (pichani) amewataka wasanii kufanya kazi nzuri ambazo
zinaweza kuwaweka sehemu nzuri na siyo kutengeneza mazingira ambayo yanautia
dosari muziki wao.
“Sisi
kama BASATA tumeona hizo picha mtandaoni, siyo kitu kizuri, kwanza hakiendani
na tamaduni zetu. Kwahiyo sisi tunamtafuta Ben Pol halafu tumsikilize, atueleze
zile picha ilikuwaje mpaka zikasambaa mitandaoni. Tukiongea naye tunaweza kutoa
kauli yoyote na kulaani matukio ya namna hiyo,”
Pia
naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza
kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la
akili au maadili limemkumba Ben Pol,” alisema Mngereza.
Pia
Mngereza amewaomba wasanii wa Tanzania kwa upande wa muziki wafanye muziki
mzuri wasitegemee kiki.
No comments