Header Ads

Wadukuzi waishambulia tovuti ya rais wa Ukraine



Tovuti rasmi ya rais wa Ukraine Petro Poroshenko imeshambuliwa na wahalifu wa mtandaoni kutoka Urusi, mamlaka yake imesema.
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko
KIEV, Ukraine
MAMLAKA ya usalama wa mtandaoni Ikulu nchini, imeeleza kuwa tovuti rasmi ya Rais Petro Poroshenko, imeshambuliwa na wahalifu wa mtandaoni kutoka Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka hiyo, hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Rais Poroshenko kupiga marufuku mitandao ya kijamii ya Urusi ambayo ni maarufu nchini. Hata hivyo, hakuna ushahidi wowote uliotolewa unaoihusisha Urusi na uvamizi huo.
Urusi haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo ya Ukraine. Utawala wa Rais Poroshenko umesema kuwa, hali hiyo ‘imedhibitiwa’ na hakuna tishio lolote katika kazi ya tovuti hiyo.
Saa kadhaa baada taarifa ya utawala huo, tovuti hiyo ilianza kufanya kazi kama kawaida huku viunganishi vyote vya habari katika ukurasa wa kwanza vikipatikana.
Uamuzi wa Serikali kupiga marufuku mitandao hiyo ya Urusi mapema jana, ni mojwapo ya hatua ya kuiwekea vikwazo Urusi kwa kuiteka Crimea 2014 mbali na madai ya kuhusika na mzozo unaoendelea Mashariki nchini.
Mitandao iliyolengwa ni pamoja na Vk.com na Odnoklassniki, Mtandao wa kutafuta, Yandex na huduma za barua pepe za Mail.ru. Kampuni za huduma za mitandao zimeagizwa kufunga mitandao hiyo.
Mali zilizopo katika ofisi za kampuni hizo nchini, zimepigwa tanji na kuwekewa vikwazo ijapokuwa haijulikani marufuku ya huduma hizo itatekelezwa vipi na iwapo Serikali ina uwezo wa kuitekeleza.
Hatua hiyo ya Rais poroshenko, ambayo ilipendekezwa na baraza la usalama la taifa, huenda ikawaathiri raia wengi kwa kuwa takriban raia milioni 14 wanatumia mtandao wa VK huku ule wa Odnoklassniki ukimaanisha waliosoma katika darasa moja ni maarufu.


No comments

Powered by Blogger.