Header Ads

Mauaji ya mwandishi yazua maandamano Mexico



Valdez alipigwa risasi katika mji huu wa Culiacan
SINALOA, Mexico
MAANDAMANO makubwa yanashuhudiwa kote nchini, baada ya mauaji ya mwaandishi maarufu wa habari za upekuzi, na mshindi wa tuzo mbalimbali, Havier Valdez, ambaye alitumia miaka mingi kufichua taarifa za magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya.

Waandhishi habari katika mjini Mexico City, waliwasilisha stakabadhi kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa nchi, wakitaka ulinzi zaidi na haki itendeke kwa waandishi watano ambao tayari wameuawa katika kipindi cha miezi kadhaa ya mwaka huu.
Vyombo vya habari na watetezi wa haki za binadamu nchini, wameungana na kuwa kitu kimoja kinachopinga tukio hilo. Valdez aliandika kwa upana kuhusu watumiaji wa madawa, na Rais Enrique Pena Nieto ametaja kifo chake kama kosa la kikatili.
Mara kwa mara walichapisha sura ya Valdez ambae aliuawa karibu na ofisi za gazeti na alipatikana nyumbani kwake Culiacan katika jiji la Sinaloa.
Mexico inatajwa kama nchi ya tatu hatari zaidi kwa usalama wa waandishi wa habari duniani, huku waandishi watano wakiwa wameuawa mwaka huu.


No comments

Powered by Blogger.