UTAFITI: Ngozi ya Samaki kutumika kuponya majeraha ya moto

SAO PAOLO, Brazil
MADAKTARI wa Brazil
wameanza kutumia ngozi ya samaki aina ya Tilapia kutibu majeraha ya moto,
wakisema kuwa ngozi ya samaki ina kiwango kikubwa cha madini ya collagen na
protein ambayo husaidia majeraha makubwa ya moto kupona haraka na kwa ufanisi.
Wanasayansi hao wameanza rasmi kutumia njia hiyo inayodaiwa kuwa na ufanisi
mkubwa zaidi ya kutumia bendeji za kawaida, kwa kuwa ngozi ya Samaki hao
inasaidia kupambana na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia majeraha ya moto
ikiwa na madini yanayosaidia kufuta alama za kuungua kwa haraka.

Inaelezwa mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 56 waliotibiwa kwa kutumia ngozi ya
Samaki hao wameonesha maendeleo mazuri. Kwa mujibu wa madaktari hao ngozi
ya Nguruwe pia inaweza kutumika kufungia vidonda vinavyotokana na moto kutokana
na kiwango kikubwa cha collage iliyopo kwenye ngozi hiyo.
No comments