Ujumbe za Zari wazua gumzo mitandaoni
UJUMBE wa mwanamama ambaye kwa sasa ni mzazi
mwenzake staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, Zari Hassan umezua tafrani
kwenye mitandao ya kijamii.
Ujmbe huo ambao mama Tiffa aliupost Jumatatu,
ulisomeka “These two days have been difficult for me. Let us pray for Ivan”
ukiwa na maana sawa na ‘Siku mbili hizi zimekuwa ngumu kwangu. Sote tumuombee
Ivan’ umegeuka kuwa gumzo licha ya mwenyewe kuupost kwa nia njema.
Gumzo hilo linakuja katika kipindi ambacho
aliyekuwa mumewe Zari, Ivan Ssemwanga alikutwa akiwa hajitambui na kulazimika kukimbizwa hospitali ya
Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya wachangiaji walijikuta wakizozana
kutokana na wengine kudai kuwa, ujumbe wake ni dharau kubwa kwa supastaa wa
Tanzania, Diamond.
“Kusema kuwa siku mbili hizi zimekuwa ngumu kwake,
ni dharau kwa Diamond ambaye kwa sasa yuko naye” alisema mchangiaji mmoja.
Mchangiaji mwingine alisema ujumbe wa kumwombea
mzazi mwenzake wa zamani si mbaya, ila ubaya unakuja pale Zari anaposema kuwa
siku hizo zimekuwa ngumu kwake.
“Ameonesha kumjali mzazi mwenzake huyo wa zamani,
lakini kaenda mbali zaidi alipodai kuwa siku hizo zimekuwa ngumu kwake” alisema
mchangiaji huyo.
Hata hivyo, wachangiaji wengine walisema kuwa
ujumbe huo ni muhimu kwani unaonesha utu na namna mwanamama huyo alivyo makini
hasa linapokuja suala muhimu la afya ya mzazi mwenzake huyo.
Mbali na kuandika ujumbe huo, Zari pia
aliambatanisha picha yake alipomtembelea Ivan hospitalini hapo alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Chanzo: Burudani Kilasiku
No comments