Polisi kuchunguza mlolongo wa mauaji ya wanawake Afrika Kusini
Mmoja wa wanawake waliouawa, Karabo Mokoena
POLISI
nchini, wanachunguza misururu mauaji ya wanawake kwenye mtaa wa Soweto jijini hapa
pamoja na mitaa ya Gauteng ambako nako miili mingine ilikutwa mwishoni mwa wiki.
Miili mitatu
tayari imetambuliwa. Baadhi ya watu ambao walitambuliwa ni, Bongeka Phungula na
Popi Qwabe ambao walidaiwa kutoweka siku ya Ijumaa na inaripotiwa kuwa pia walibakwa.
Mwili wa
Lerato Moloi ulipatikana eneo la Naledi huko Soweto, huku mwili wa nne
ukipatikana eneo linalotumika kutupa taka.
Radio mbalimbali
hapa nchini, zimepokea simu nyingi kutoka kwa raia wanaoitaka Serikali kuchukua
hatua ya kupambana na uhalifu na kufanya jitihada za kuwalinda wanawake na
watoto.
No comments